Habari 5 Kubwa Za Soka Jumanne Mei 26

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne Mei 26

1. Everton imewasilisha ombi la £40m kumsaini kiungo wa kati wa Napoli, Allan, 29, lakini klabu hiyo inataka dau la £60m kumuuza raia huyo wa Brazil.

2. The Toffees pia wamewasilisha ombi la $25m kwa Barcelona kumnunua beki wa Ufaransa Jean -Claire Todibo ,20, ambaye kwa sasa anahudumu kwa mkopo katika klabu ya Schalke nchini Ujerumani.

3. Manchester United itamuongezea kandarasi kipa wa England Dean Henderson, 23 ili kumruhusi kumaliza msimu wake na klabu ya Sheffield United huku kandarasi yake ikitarajiwa kukamilika mwezi Juni.

4. Mmiliki wa Bournemouth Maxim Demin karibu aiuze klabu hiyo kwa mfanyabiashara wa Saudia mnamo mwezi Januari , kabla ya makubaliano hayo kugonga mwamba kuhusiana na thamani ya klabu hiyo.

5. Kiungo wa kati wa Brazil Phillipe Coutinho ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Bayern Munich huenda asicheze tena baada ya klabu hiyo ya Bundesliga kuamua kutomsaini kwa mktaba wa kudumu kutoka Barcelona, na sasa ananyatiwa na Chelsea, Arsenal na Tottenham.


EmoticonEmoticon