Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatano May 13

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Jumatano May 13

1. Newcastle wako tayari kutumia £53m kumpata mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale, 30, mpango ambao ukifanikiwa utamrejesha nyota huyo katika ligi kuu ya England msimu huu.

2. Tottenham haitakubali Tanguy Ndombele, 23, kuondoka klabu hiyo msimu huu. Kiungo huyo wa kati wa Mfaransa amehusishwa na tetesi za kujiunga na Barcelona na Liverpool.

3. Manchester United wanataka kuwasajili wachezaji watatu wa Uingereza msimu huu akiwamo- mshambuliaji wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 20, kiungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish, 24, na kiungo wa kati wa Birmingham wa miaka 16, Jude Bellingham. 

4. Juventus wamekuwa klabu ya kwanza ya Italia kuweka kanuni ya mshahara kwa wachezaji wake, hatua ambayo imewafanya kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba,27.

5. Lionel Messi, 32, na baadhi ya wachezaji wenzake nchini Uhispania huenda wakapunguziwa mshahara kwa asilimia 30 msimu ujao huku Barcelona na Real Madrid wakitathmini hatua ya kupunguza marupurupu ya wachezaji kutokana na athari iliyosababishwa na virusi vya corona.


EmoticonEmoticon