Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatano May 6

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Jumatano May 6

1. Manchester United wako makini kumsajili kiungo wa kati wa Juventus na Wales Aaron Ramsey, 29, kama sehemu ya makubaliano ya mabadilishano na mchezaji wa Ufaransa Paul Pogba, 27.

2. Winga wa Chelsea Willian, 31, anatarajiwa kusalia London mkataba wake Stamford Bridge utakapofikia ukomo Juni, huku mchezaji huyo wa Brazil akitarajia kuungana na kocha wake wa zamani Jose Mourinho at Tottenham.

3. Juventus itaendelea na azma yake ya kumwinda winga wa Italia Fiorentina Federico Chiesa, wakati ambapo klabu yake iko tayari kumuuza kwa tahamani yake anastahili huku Chelsea, Manchester United pamoja na Inter Milan pia nao wakiwa wanammezea mate mchezaji huyo, 22.

4. Matumaini ya Everton kumsajili mchezaji wa Napoli Allan, 29, yanadidimia wakati ambapo mmiliki wa klabu hiyo ya Serie A akisema thamani ya kiungo wa kati wa Brazil ya euro milioni 65 ikitarajiwa kupungua kwasababu ya Covid-19 - sawa na ilivyo kwa mchezaji mlinzi wa Senegali Kalidou Koulibaly, 28, anayelengwa na Liverpool anayesemekana kuwa na thamani ya euro milioni 95.

5. Msambulizi wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 21, ameomba kuruhusiwa kuhama timu hiyo kwenda Real Madrid au klabu nyengine yoyote ya Ulaya siku za usoni.


EmoticonEmoticon