Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatano Mei 20

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Jumatano Mei 20
1. Manchester United inapigiwa upatu kumnyakua winga wa Wolverhampton Wanderers Adama Traore, hata hivyo United itachuana na Liverpool na Manchester City katika mbio za kumsajili mchezaji huyo mwenye miaka 22.
2. Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 19 alikataa mpango wa kuhamia Juventus mwezi Januari kwa kuwa timu hiyo ilikuwa na mpango wa kumjumuisha katika kikosi cha wachezaji wa umri wa chini ya miaka 23.
3. Mshambuliaji wa Manchester City Leroy Sane hana mpango wa kuhamia kwa mahasimu wao katika ligi ya primia, Liverpool. Mchezaji huyo, 24 raia wa Ujerumani anaendelea kujiandaa kuhamia Bayern Munich.


4. Arsenal wana matumaini ya kumsajili winga anayechezea kikosi cha wachezaji wa umri wa chini ya miaka 21, katika klabu ya Bayer Leverkusen Moussa Diaby. Kinda huyo, mwenye 20 ambaye ni mchezaji wa zamani wa Paris St-Germain alitengeneza magoli mawili katika ushindi wa Leverkusen dhidi ya Werder Bremen siku ya Jumatatu.

5. Chelsea wanaongoza katika mbio za usajili wa beki wa kati wa kiholanzi Xavier Mbuyamba, 18, kutoka kwa miamba ya Uhispania Barcelona, hayo ni kwa mujibu wa wakala wa kinda huyo.


EmoticonEmoticon