Habari 5 Kubwa Za Soka Jumanne May 12

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Jumanne May 12
1. Mchezaji nyota wa Arsenal Mesut Ozil, 31, hataondoka klabu hiyo msimu huu na badala yake atakamilisha mwaka mmoja uliosalia katika mkataba wake na Gunners . (Fanatik, via Football London)
2. Arsenal wanamatumaini ya kusalia na kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos, 23, kwa mkopo hadi msimu wa sasa wa ligi ya primia utakapo kamilika, lakini wanapanga kurefusha mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania katika klabu hiyo kwa msimu mwingine. 
3. Manchester United wanataka kumsaini kiungo mahiri wa Argentina Thiago Almada, 19, ambaye pia ananyatiwa na Arsenal, kutoka Velez Sarsfield. Pia Man U bado hawajakubaliana kuhusu mkataba mpya na kiungo wa kati Angel Gomes,19, ambaye mkataba wake wa sasa unakamilika mwisho wa Juni.
4. Chelsea wana amini watampata Charlie Webster, ambaye anaripotiwa kunyatiwa na Borussia Dortmund, katika mkataba wa wa kitaalamu atakapofikisha miaka 17 Januari ijayo.
5. RB Leipzig wameungana na Everton katika kinyang'anyiro cha kumsaka beki wa Ufaransa wa miaka 20- Jean-Clair Todibo kutoka Barcelona. 


EmoticonEmoticon