Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatatu Mei 18

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Jumatatu Mei 18
1. Manchester United watapaswa kulipa pauni milioni 80 kwa ajili ya kumnasa kiungo wa Aston Villa Jack Grealish, 24, hata kama timu yake itashuka daraja msimu huu.
2. Kiungo wa kati wa Bayern Munich Corentin Tolisso pia analengwa kusajiliwa na klabu ya Manchester United. Bayern iko tayari kumuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa 25 kwa ajili ya kupata fedha ili kununua wachezaji wengine, akiwemo winga wa Manchester City mjerumani Leroy Sane, 24.
3. Juventus itakuwa kwenye kinyang'anyiro na Manchester United kumnasa mshambuliaji wa Wolves Raul Jimenez, 29. 
4. Winga wa Bournemouth na Scotland Ryan Fraser,26, anaaminika kuwa anapenda kujiunga na Tottenham kwa uhamisho wa bure punde tu baada ya mkataba wake na kbalu yake ya sasa utakapokamilika tarehe 30 mwezi Juni. (Mirror)
5. Kiungo wa kati wa Liverpool Pedro Chirivella,22, amepewa ofa ya mkataba wa miaka mitano lakini hajaamua bado kuhusu mustakabali wake, tayari klabu za Nates na Rangers wameonesha kuwa na nia ya kumchukua.


EmoticonEmoticon