Instagram Kuanza Kuwalipa Wateja Wake Kwa Kupitia Video Za IGTV

Kampuni ya Instagram ipo mbioni kuanza kuweka matangazo kwenye video za IGTV , na kuwapa fursa watumiaji wake kuanza kutengeneza pesa .

Kwa mujibu wa Hollywood Report , kampuni hiyo inataka kutambulisha Updates na Features mpya ambazo zinawanufaisha na kuwafanya watumiaji wake wajitengenezee pesa Kama ilivyo kwa YouTube .

Moja Kati ya mabadiliko hayo makubwa , ni pamoja na kuweka matangazo kwenye video ndefu zinazozidi sekunde 60 (InstagramTv) . Pamoja na Beji za makampuni kwenye Insta Live , ambazo zitamfanya aliyeweka video hizo kulipwa.


EmoticonEmoticon