Italia Itaanza Kulegeza Masharti Ya Usafiri Na Marufuku Ya Kutotoka Nje

Serikali ya Italia imeweka saini amri itakayoruhusu usafiri wa kuingia na kutoka nchini humo kuanzia Juni 3, inapojiandaa kulegeza marufuku ya kutotoka nje iliyowekwa kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona.
Taifa hilo pia litaruhusu usafiri kati ya maeneo - ambayo kulikuwa kumedhibitiwa kuanzia siku hiyo.
Uamuzi huo unaashiria hatua kubwa katika juhudi za nchi hiyo kufungua tena uchumi wake baada ya zaidi ya miezi miwili ya kufungwa.
Italia ina moja ya viwango vya juu zaidi vya vifo vilivyotokana na ugonjwa wa corona ulimwenguni, lakini kiwango cha maambukizo kimepungua katika siku za hivi karibuni.
Zaidi ya watu 31,600 walifariki katakana na virus vya corona nichini humo, idadi ambayo ni ya tatu kwa ukubwa nyuma ya Marekani na Uingereza.


EmoticonEmoticon