Kampuni Ya Rolls-Royce Kupunguza Wafanyakazi Zaidi Ya 8,000

Kampuni ya Rolls-Royce ya nchini Uingereza imetangaza kupunguza Wafanyakazi 9,000 baada ya soko lao kuumizwa vibaya na Janga la Corona.
Kampuni hiyo ambayo hutengeneza Injini za ndege imesema hatua hiyo itaokoa takribani shilingi Trilioni 3.6 za Kitanzania.
Pia wametoa angalizo kwamba inaweza kuwachukua miaka kadhaa kwa soko lao la biashara ya vifaa vya ndege kuweza kurudi kwenye hali yao ya zamani.
Msemaji wa kampuni hiyo amesema idadi hiyo ya wafanyakazi itapunguzwa toka kwenye idadi ya wafanyakazi 52,000 waliopo duniani kote.


EmoticonEmoticon