Kenya kufanyia majaribio chanjo ya Covid-19 kwa binadamu

Wanasayansi wa Kenya wameungana na wenzao wa kimataifa katika juhudi za kutafuta chanjo ya ugonjwa wa Covid-19, kwa kufanyia majaribio dawa tatu.
Majaribio ya chanjo itafanyiwa binadamu ili kubaini ikiwa dawa hizo zinaweza kutibu ugonjwa huo.
Lakini Je dawa hizo ni zipi?
Watafiti wamekuwa mbioni kupata idhini ya kufanyia majaribio ya dawa aina tatu ikiwa ni pamoja na:
§  Remdesivir, ambayo iliidhinishwa na Marekani kama dawa ya dharura ya kutibu Covid-19.
§  Dawa ya kutibu malaria ya hydroxychloroquine.
§  Lopinavir/ritonavir, ambayo pia inatumiwa na wagonjwa wa HIV.
Kwa mujibu wa Gazeti la Nation nchini Kenya mtafiti mkuu katika uchunguzi huo Dkt Loice Achieng Ombajo, ambaye ni mkuu wa kitengo cha magonjwa ya kuambukiza katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta amesema kwamba kufikia sasa hakuna tiba ya Covid-19 inayopewa mgonjwa.
Badala yake ,wagonjwa wanasadiwa kukabiliana na dalili zinazoonekana kama vile kuwa na homa kali na kuumwa na videnda vya koo.
Kenya imefika wapi katika majaribio hayo?
''Tuko katika awamu amabapo hatuwezi kubaini moja kwa moja nini kinafanya kazi'' alisema Dkt Loice Achieng Ombajo.
Aliongeza kuwa katika majaribio ya tiba wagonjwa wengi wanashirikishwa bila mpangilio maalu lakini wote wanapewa dawa tofauti na wenzao.
''Kuna uwezekano wa dawa moja ikafanya kazi lakini wataalamu wanatakiwa kufuatilia kwa makini mienendo ya mgonjwa," alisema katika mahojiano na gazeti la Nation.
Kufikia sasa Dkt Ombajo, na wenzake wamepata idhini kutoka kwa kamati ya maadili ya Chuo Kikuu cha Nairobi na mapendekezo yao kuchunguzwa na bodi ya dawa nchini Kenya.
Watafiti hao kwa sasa wanasubiri tamko la mwisho kutoka kwa bodi hiyo na Baraza la kitaifa la Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (NACOSTI).
Hatua nyingine muhimu kwa mujibu wa watalamu hao, ni kuhamasisha umma kuhusu majaribio hayo ya tiba kabla ya watu ''kufanya maamuzi'' ikiwa wanataka kushiriki katika zoezi.
Credit:bbc


EmoticonEmoticon