Kenya Yafunga Mipaka Yake Tanzania Na Somalia, Muda Wa Kukaa Ndani Waongezwa, Wagonjwa Corona Jumla 830

Kenya imefunga kwa muda wa siku 30 mipaka yake ya kimataifa kuenda Tanzania na Somalia kuanzia saa sita usiku wa Jumamosi Mei 16.
Katika hotuba yake kwa taifa Rais Uhuru Kenyatta amesema hatua hiyo inajumuisha udhibiti usafiri wa watu kutoka mataifa hayo kuingia nchini Kenya.
Hatahivyo usafirishaji wa mizigo utaindelea kati ya Kenya na mataifa hayo mawili.
Marufuku hiyo ya kuzuia watu kutoka Tanzania na kuingia nchini Kenya inaanza usiku wa leo saa 6 na kuruhusu mizigo tu kupita.
Na kwa upande wa Somalia masharti ni hayo hayo, mizigo peke yake ndio itaruhusiwa.
Aidha madereva watakaoingia nchini Kenya kuleta mizigo watatakiwa kupima corona kwanza.
Kenya imeongeza tena muda wa marufuku ya kutoka nje kwa muda wa siku 21.
Kufikia sasa idadi ya watu walioambukizwa na virusi vya corona nchini Kenya imeongezeka hadi 830 baada wagonjwa wapya 49 kuthibitishwa kuwa na ugonjwa huo.
Waliofariki kutokana na corona ni watu 50 baada ya wengine watano kufa.
Rais Kenyata pia ametangaza kuwa wagonjwa 17 wametolewa hospitalini walipokuwa wakipata matibabu.
Credit:Bbc


EmoticonEmoticon