CORONA : Kenya Yasajili Idadi Kubwa Visa Vipya 72 Kwa Siku Moja, Jumla Visa 1,282

Kwa mara ya kwanza Kenya imesajili visa vingi vya maambukizi vikiwa 72 baada ya watu 2,711kufanyiwa vipimo na kufikisha watu walioathirika kuwa 1282.

Wakati uo huo watu 9 wameruhusiwa kutoka hospitalini na kufikisha watu 402 waliopona ugonjwa huo.

Aidha katibu msimamizi Mercy mwangangi amesema mtu mmoja amepoteza maisha yake na kufikisha wale walioaga nchini kuwa 52.

Kati ya watu 72 waliopatikana na virusi hivyo hii leo.Mwangangi amesema 70 ni wakenya huku mmoja akiwa raia wa kigeni.

Waathiriwa siku ya jana ni kati ya umri wa miaka 12 hadi 78. Kaunti ya Nairobi imesajili visa 52 kati ya visa vipya vilivyosajiliwa siku ya jana.

Kufikia sasa serikali ya Kenya imeweza kuwapima wakenya 61,971 kwa ujumla.
Credit:Radiojambo


EmoticonEmoticon