Kenya Yasajili Idadi Ya Juu Maambukizi Ya Corona 123 Jumla 1,471

Kwa mara ya kwanza nchini, Kenya imesajili idadi ya juu zaidi ya watu walioambukizwa na virusi vya corona wakiwa watu 123 na kufikisha idadi  nchini humo kuwa 1,471.

Kaunti ya Nairobi iliandikisha visa 78 huku kaunti ya Mombasa ikiwa na visa 45 kati ya visa hivyo 123.

Kufikia sasa, Mutahi amesema wagonjwa 7 wako katika hali mahututi na wamewekwa chini ya mashine ya kuwasaidia kupumua.

Ameongezea kuwa watu watatu zaidi wamefariki na kufikisha idadi ya watu walioaga nchini humo kuwa watu 55.
Watu hao 123 walipatikana baada ya serikali kufanyia watu 3077 vipimo.

Mutahi amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na serikali na kufuata masharti ambayo serikali imeweka ili kupunguza maambukizi zaidi.
Credit:Radiojambo


EmoticonEmoticon