Kenya Yatangaza Maambukizi Mapya Ya Wagonjwa Wa Corona 57, Jumla 887

Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona nchini Kenya imeongezeka hadi kufikia 887 baada ya wagonjwa wengine 57 kukutwa na virusi hivyo katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
Wagonjwa hao ni wanawake 23 na wanaume 34 wote wakiwa kati ya umri wa miaka miwili na 61.
Katika taarifa iliotolewa na wizara ya Afya siku ya Jumapili, Msemaji wa serikali Cyrus Oguna alisema kwamba kati ya wagonjwa hao wapya mjini Mombasa , Nairobi 17 , kajiado 3 huku Kwale na Kitui zikitangaza wagonjwa mmoja mmoja mtawalia.
Wagonjwa hao wapya walipatikana baada ya smapuli 2198 zilzipimwa. Kufikia sasa taifa hilo limefanikiwa kupima watu 43,712.


EmoticonEmoticon