Kituo Cha Misaada Cha Watoto Chakataa Milion 465 Kutoka Kwa Rapa Tekashi69

Baada ya GOOBA kuendelea kufanya vizuri kwenye mitandao mbali mbali na kuweka rekodi kubwa, Tekashi69 aliamua kufanya jambo la kuisadia jamii yake.

Rapa huyo mtata aliripotiwa kutaka kuchangia kiasi cha ($200k) sawa na TSH. Milioni 465 kwa kituo/taasisi inayojihusisha na masuala ya watoto iitwayo, No Kid Hungry.

Baada ya taarifa hizo kusambaa, haikuchukua muda kwa taasisi hiyo kuibuka na waraka wa kutamka kuzitema pesa hizo na kukataa msaada wa rapa huyo mtukutu. Wameeleza

"Tumejisikia fahari kwa juhudi za Bwana Hernandez kutaka kusaidia kituo chetu cha No Kid Hungry lakini tumewajulisha wawakilishi wake kwamba tumeukataa msaada huo. Ni sera yetu kukataa misaada kutoka kwa wachangiaji ambao shughuli zao hazilandani na malengo pia maadili ya taasisi yetu."

Tamko hilo lilimfikia 69 na kujibu kwamba "No Hungry Kid wameona bora wawapore tonge mdomoni hawa watoto wasio na hatia, sijawahi kuona kitu cha kikatili kama hiki."


EmoticonEmoticon