Kubadilika Umbo Kwa Virusi Vya Corona: Fumbo Kwa Wanasayansi Juu Ya Athari Za Virusi

Watafiti nchini Marekani na Uingereza watambua mamia ya mabadiliko ya maumbile ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.
Lakini hakuna hata mmoja ambaye amefahamu ambacho hii itamaanisha katika kusambaa kwa virusi miongoni mwa watu na ikiwa chanjo itakua na ufanisi.
Virusi vinabadilika maumbile-hicho ndicho kinachotokea.
Tatizo ni: aina gani ya maumbile haya yanayoleta mabadiliko ya kuufanya ugonjwa uwe mbaya zaidi au kuyafanya maambukizi kuwa ugonjwa?
Utafiti wa awali kutoka Marekani umeelezea kuhusu moja ya mabadiliko ya kimaumbile uliouita - D614G - ambayo yamejitokeza zaidi na huenda kukasababisha maambukizi makali zaidi.
Hatahivyo bado haujatathminiwa na wanasayansi wengine na kuchapishwa rasmi.
Watafiti, kutoka Maabara ya Los Alamos National Laboratory nchini New Mexico, wamekua wakifuatilia mabadiliko hadi kufikia "tawi" la kirusi yanayoleta mabadiliko ya kipekee ya kimaumbile, kwa kutumia mfumo wa data uliopangwa unaoitwa Global Initiative on Sharing All Influenza Data (GISAID).
Walibaini kuwa inaelekea kuna kitu fulani kuhusu mabadiliko hayo ya kimaumbile yanayokifanya kirusi kukua haraka zaidi - lakini athari za mabadiliko haya bado hazijawa wazi.
Timu ya utafiti iliyotathmini data za Uingereza kutoka kwa wagonjwa wa virusi vya corona katika eneo la Sheffield.
Ingawa walibaini kuwa watu wenye virusi hivyo vinavyobadilika umbo walionekana kuwa na kiwango kikubwa cha virusi katika sampuli zao za vipimo, hawakupata ushahidi wa wazi kwamba watu wale waliugua au walilazwa hospitalini kwa muda mrefu.
Chanzo:Bbc


EmoticonEmoticon