Kwa Saa 24 Dunia Yaandikisha Maambukizi Makubwa Zaidi Ya Wagonjwa Wa Corona

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameonya kwamba janga virusi vya corona bado ni safari ndefu licha ya kwamba wanaoathirika wanaendelea kuongezeka kote duniani kila uchao.
WHO imesema kwamba waathirika wapya 106,000 wameripotiwa katika shirika hilo ndani ya kipindi cha saa 24 zilizopita.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameonesha wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa maambukizi katika mataifa ya kipato cha chini na cha wastani.
Onyo hilo linawadia huku idadi jumla ikikaribia kufika milioni tano.
Idadi hiyo ya kusikitisha inafikiwa chini ya wiki mbili baada ya ya kurekodiwa maambukizo milioni nne kote duniani.
Wataalamu wameonya kwamba idadi kamili ya maambukizi huenda ikawa ya juu zaidi na idadi ya wanaopimwa ni ya chini katika nchi nyingi ambazo wanaficha taarifa zao.
Zaidi ya watu 326,000 wanakadiriwa kuwa wamekufa kwa virusi vya corona kote duniani kulingana na chuo kikuu cha Johns Hopkins.
Marekani bado ndio iliyoathirika zaidi ikiwa na walioambukizwa milioni 1.5 na idadi ya waliokufa ikifikia 92,000.
"Katika kipindi cha saa 24 zilizopita, kumekuwa na maambukizo mapya 106,000 ambayo yameripotiwa kwa WHO - ambayo ni makubwa zaidi kuandikishwa kwa siku moja toka janga la corona lianze," Dkt Tedros aliwaeleza wanahabari Jumatano jioni.
"Karibia theluthi mbili ya walioathirika wameripotiwa katika nchi nne pekee," aliongeza.
Dkt. Tedros baadae alionya kwamba dunia kwamba safari ya kupambana na janga hili bado ni ndefu.
Onyo lake linawadia wakati ambao mataifa kadhaa kama vile Marekani imeanza kulegeza masharti.
Credit:Bbc


EmoticonEmoticon