Kwa Siku Moja Kenya Imesajili Visa 45 Vya Wagonjwa Wa Corona

Kwa mara nyingine tena taifa la Kenya limesajili idadi kubwa zaidi ya maambukizi Afrika Mashariki baada ya watu 45 kupatikana na virusi hivyo nchini.

Akitoa tangazo hilo waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema watu hao walipatikana baada ya sampuli za watu 1777 kufanyiwa vipimo.

Kati ya watu hao 45, 29 ni kutoka kaunti ya Nairobi, 11 Mombasa, 5 Wajir.

Aidha Kagwe amesema kuwa watu wengine 9 wameruhusiwa kutoka hospitalini na kufikisha watu 182 waliopona nchini.
Aidha eneo la Mombasa kwa jina Old Town ambapo jamaa walikataa kupimwa lilirekodi visa 39 kufikia sasa.

Kati ya watu hao 45, 30 ni wanaume na 15 wakiwa wanawake.
Mutahi amesema visa 29 vilivyoripotiwa nchini vimetokea katika eneo la Eastleigh jijini Nairobi.

Mutahi vile vile amesifia hatua ya gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho ambaye amemtaja kuwa kipaumbele kwa kuhamasisha umma kuanza kufanyiwa vipimo.

Aidha Mutahi amewataka wakenya kuzingatia masharti yaliyowekwa na serikali na kusema kuwa serikali sasa imeanza kupania kuongeza vigezo vingine.

Mutahi ameshikilia kiki kuwa ni lazima madereva wa masafa marefu kufanyiwa vipimo ndiposa wakaruhusiwa kuingia nchini.
credit:radiojambo


EmoticonEmoticon