Licha ya Uwepo Wa janga La Corona, Tuzo Za BET Mwaka Huu Zimetajwa Kuwa Zitafanyika

Waandaaji wa tuzo hizo wametoa tamko la kuendelea na programu hiyo ambayo itafanyika June 28 mwaka huu. 

Lakini kulingana na kanuni za kuepusha mikusanyiko, BET wametangaza kuifanya hafla hiyo katika namna ya kipekee, wamesema watatumia njia za kibunifu za Kiteknolojia pamoja na maudhui ambayo yatatengenezwa na wasanii wenyewe ili kumfanya mtazamaji na hata msanii na wadau wengine wajihisi kama wapo pamoja ukumbini. Kitaalamu wanaita "Virtually"

Katika tuzo za mwaka huu zitakuwa za 20 tangu zianzishwe pia itakuwa ni hafla ya kusherehekea miaka 40 ya kuanzishwa kwa kituo cha BET (Black Entertainment Television)

Bado haijafahamika ni lini maijna ya wasanii washiriki yatatajwa au nani atashiriki katika tuzo hizo za mwaka huu ambazo zitakuwa za namna yake.


EmoticonEmoticon