Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) Haitorejea Tena May 15, Tarehe Nyingine Yatajwa


Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) sasa itarejea May 22 na sio 15 kama ilivyoripotiwa awali sababu ya Chancellor wa Ujerumani Angel Merkel kuagiza kuwa soka Ujerumani litarejea timu za madaraja yote zikimaliza karantini ya siku 14.
Leo iliripotiwa kuwa viongozi wa juu wa serikali ya Ujerumani watakaa na kutangaza uamuzi ambao utakuwa salama kwa Ligi Kurejea pasipo kuleta madhara.
Vikosi vya timu za Bundesliga vilishaanza mazoezi tayari wiki iliyopita ikiwa ndio mara ya kwanza toka March 8 2020 pale Ligi iliposimamishwa.


EmoticonEmoticon