Ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga Kurejea Mei 16 Bila Mashabiki Uwanjani, Watu 300 Wataruhusiwa


Ligi kuu ya Ujerumani maarufu ,Bundesliga itarejelea mechi zake bila kuwa na mashabiki uwanjani tarehe 16 Mei.
Hiyo itakuwa mechi ya kwanza kuchezwa katika ligi la Ulaya kufuatia mechi nyingi kusitishwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.
Moja ya michuano ambayo itachukua nafasi ni kati ya timu ya Schalke na Borussia Dortmund.
Mabingwa wa ligi hiyo Bayern Munich, ambao wanaongoza kwa alama nne kusawazisha kuingia kiwango cha juu, pale watakapokutana kwenye mechi mjini Berlin siku ya Jumapili.
Timu nyingi zina michezo tisa ya kucheza, na msimu huu fainali zinatarajiwa mwishoni mwa wiki ya tarehe 27-28 Juni.
Shirikisho la soka nchini Ujerumani (DFB) alisema msimu huu utaanza huku kukiwa na masharti ya kiafya ambayo lazima yazingatiwe kwa kutoruhusu mashabiki kuhudhuria uwanjani kuona mechi na wachezaji kupima virusi vya corona.
Watu wapatao 300 wakiwemo wachezaji, wafanyakazi na maofisa ndio watakuwa ndani au karibu na uwanja wa mpira, siku mechi itakapochezwa.


EmoticonEmoticon