Ligi Ya EPL inategemewa Kurejea June Mwaka Huu

Pazia la ligi hiyo litafunguliwa kwa mechi mbili, mtanange baina ya Manchester City dhidi ya Arsenal na Aston Villa dhidi ya Sheffield United.
Mechi hizo mbili ni za viporo. Ratiba kamili itaanza wikiendi ya Juni 19-21.
Klabu zinazoshiriki ligi hiyo bado zinaendelea na mjadala wa namna ya kurejea kwa ligi katika mkutano unaoendelea hii leo, na inaelezwa kuwa kufikia sasa wanakubaliana juu ya tarehe hizo.
Bado kuna jumla ya mechi 92 ambazo zinahitaji kuchezwa na vilabu vyote 20.
Ligi ya EPL ilisimamishwa kwa muda usiojulikana Machi 13 kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.
Siku ambayo ligi itarejea itakuwa ni kilele cha siku 100 kamili toka mechi yake ya mwisho ambapo Leicester City iliitandika 4-0 Aston Villa.
Tofauti kubwa yah apo awali na sasa ni kuwa ligi hiyo itarejea bila kuwa na mashabiki uwanjani.


EmoticonEmoticon