Majibizano Ya Meek Mill Na Tekashi 6ix9ine, Rekodi Mpya Ya Takesh Ipo Hapa


Rapa Meek mill amemshambulia TEKASHI 6ix9ine Kwa kumuita Panya , huku akimtaka aombe radhi kwa kuwachoma/Snitch kundi lake mahakamani , ili aweze kuruhusiwa kutoka Jela

Meek ametumia mtandao wake wa Twitter Kurusha makombora ya maneno kwa Tekashi , huku akijatamba kua ana pesa zaidi yake ivyo hababaika na Number za YouTube anazopata msanii huyo.
Rapa Tekashi alitangaza kwenda 'LIVE' kupitia Ukurasa wake wa Instagram siku Jana , ambapo amefanikiwa Kuvunja Rekodi kwa kufanikiwa Kutazamwa na watu zaidi ya milion 2

Masaa Machache kabla ya Tekashi hajaruka 'Live' Meek Mill kupitia Ukurasa wa Twitter aliandika - " Nategemea huyo Panya anaruka Live ili kuomba radhi kwa watu aliowachoma na kuwaumiza , Watu mnasahau haraka Sana, Panya huyu ndie aliesababisha Nippsey Hustle akauawa na kuacha mke na Mtoto"

Hata ivyo Tekashi alimjibu Meek Mill kwa kumwambia - " Inashangaza mtu ambae umepata mtoto hivi Karibuni , unaumizwa kichwa na kusumbuliwa na Mimi mtoto wa kihispania ambae Nina nywele za Rangi ya upinde wa Mvua"


EmoticonEmoticon