Makamu Wa Raisi Wa Sudani Kusini Apata Corona

Makamu wa rais wa Sudan Kusini Dkt James Wani Iga amesema kuwa amepatwa na virusi vya corona.

Akitangaza taarifa hiyo kupitia shirika la habari la taifa la Sudan Kusini amesema: ''Sampuli zangu zilichukuliwa siku chache zilizopatikana na leo nimepatikana na ccorona...kwahiyo ninawaomba raia wote wa Sudan Kusini kwenda kupimwa , hii ni muhimu ili tupunguze kusambaa kwa virusi kwa watu wengi'', amesema

Taarifa ya kupatwa kwa maambukizi ya virusi vya corona kwa Dkt James Wani Iga , inakuja baada ya viongozi wengine wakuu wa nchi hiyo kutangaza kupatwa na Covid-19 mkiwemo makamu rais wa nchi hiyo Riek Machar na mkewe pia waambukizwa virusi vya corona mwezi huu.


EmoticonEmoticon