Marekani Yawazuia Raia Wa Kigeni Kutoka Brazil

Marekani imewawekea marufuku ya usafiri raia wa kigeni ambao wamekuwa Brazil katika kipindi cha siku 14 zilizopita.
Taifa hilo la Amerika Kusini hivi karibuni limekuwa ngome la pili kuu la maambukizi ya virusi vya corona duniani.
Brazil imethibitisha kuwa zaidi ya watu 360,000 wameambukizwa corona, huku zaidi ya watu 22,000 wakifariki kutokana na baada ya wizara ya Afya ya nchi hiyo kutangaza Jumapili hali ilivyo.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani amesema kuwa udhibiti huo wa usafiri utasaidia kuhakikisha hakuna maambukizo mapya yataletwa nchini.
"Hatua ya leo itasaidia kuhakikisha raia wa kigeni ambao wamekuwa Brazil hawatakuwa chanzo cha maambukizi mapya ya corona nchini mwetu," Ilisema taarifa ya Msemaji wa Ikulu ya Marekani Kayleigh McEnany.


EmoticonEmoticon