Mike Tyson Apewa Ofa Ya Mabiliano Kurejea Uwanjani, Je Atakubali?

Jina la Mike Tyson (53) linaweza kuendelea kuandikwa zaidi kwani imetoka taarifa kwamba mbabe huyo wa zamani wa masumbwi ya uzito wa juu duniani alipewa ofa ya ($20M) sawa na Bilioni 46.2 za Kitanzania kurejea ulingoni kwa pambano moja tu.

Kwa mujibu wa MMA Fighting, bondia huyo ambaye alistaafu mwaka 2005 aliahidiwa ofa hiyo kwa pambano moja la kampuni ya ngumi iitwayo (Bare Knuckle Championship) lakini aliipiga chini.

Rais wa kampuni hiyo bwana David Feldman amesema anaamini Tyson ataikubali tu ofa yao na milango bado ipo wazi ya kukubali.

Hadi anatundika Glovu zake, Mike Tyson alikuwa amepigana mapambano 58, akishinda 50 huku 44 ikiwa kwa KO, na alipoteza mapambano 6 na mawili yakimalizika bila mshindi kwa sababu maalum.


EmoticonEmoticon