Muonekano Mpya Wa Adele Wazua Maswali Kwa Mashabiki Huku Wengine Wakimsifu

Staa wa muziki kutokea nchini Uingereza, Adele amekuwa akijadiliwa kwa sana mtandaoni kutokana na muonekano wake mpya wa sasa.

Tangu mwaka huu uanzae, Mwimbaji huyo alikuwa hajaposti picha yoyote kwenye kurasa zake za mitandao wa kijamii.

Adele ambaye mara ya mwisho alitamba na kibao chake pendwa kiitwacho Hello, amejitokeza mtandaoni na kuwashukuru mashabiki na wahudumu wa Afya kwenye siku yake ya kuzaliwa, huku akionekana akiwa na muonekano mpya au mwembamba tofauti na hapo awali.
Hata hivyo mashabiki wake wengi wamemsifia sana Staa huyo huku mashabiki wake wengine wakionyesha kushangazwa na umbo hilo.


EmoticonEmoticon