Mwanadada Aliyeibuka Na Kudai Kuwa Ni Mtoto Wa Jay zKwa Jinsi Walivyofanana

Jay-Z atakuwa baba wa watoto Wanne, kama taarifa hizi zikithibitishwa. Mwanadada mmoja ameibuka na kudai ni mtoto wa kwanza wa rapa huyo ambaye ana watoto watatu na mkewe Beyonce.

La’Teasha Macer, binti mwenye umri wa miaka 28 amefunguka kwamba amekuwa akiambiwa kwenye maisha yake yote kuwa yeye ni mtoto wa kwanza wa Jay-Z.

Kwa mujibu wa mtandao wa Bossip, Macer alizaliwa Cambridge, Maryland miaka 28 iliyopita. Inaarifiwa kwamba Shangazi yake alimtambulisha Mama yake Macer aitwaye Lisa (Kabla ya Macer kuzaliwa) kwa Jay-Z, kisha wakaanzisha mahusiano na baadaye kupata mtoto.

Baada ya kujifungua mtoto huyo (La’Teasha Macer) Lisa pamoja na familia yake walihangaika kumtafuta Jigga lakini hawakumpata na kukata tamaa.
-
"Nimekuwa kimya kwa muda mrefu, ungana nami ninapo simulia hadithi yangu ya kuishi kwenye kivuli cha kuwa binti wa Jay-Z kwenye mji ambao kila mmoja anafahamu kwamba ni Baba yangu." ameandika La’Teasha Macer kwenye ukurasa wake wa instagram.

Bado upande wa Jay-Z haujafunguka chochote hadi sasa kuhusu taarifa hizi.


EmoticonEmoticon