Mwanajeshi wa Ikulu Akutwa na Corona, Trump Na Makamu Wake Wafanyiwa Vipimo Vya Haraka Na Majibu Yametoka

Mmoja wa Wanajeshi wa Marekani ambaye anafanya kazi Ikulu ya Nchi hiyo(White House) amebainika kuwa na corona.

Mwanajeshi huyo Mwanaume ni miongoni mwa wasaidizi wa Rais Trump Ikulu ambao wanashughulika na usalama wa chakula cha Trump na Familia yake na huwa wanasafiri na Trump.

Kutokana na hali hiyo Donald Trump na Makamu wake, Mike Pence wamelazimika kupima tena maambukizi ya virusi vya corona, vipimo vimeonesha Trump na Pence ni wazima.

“Tuna vipimo bora kuliko nchi yoyote duniani, nimepima jana na leo sina corona….” amesema Trump.

Taarifa ya Ikulu (White House) imesema  pamoja na tukio hilo, rais na makamu wake wamefanyiwa uchunguzi wa afya zao na kukutwa wako katika hali njema


EmoticonEmoticon