Mwigizaji Tajiri Duaniani Tom Cruise Kucheza Filamu Nje Ya Dunia

Tarajia kuiona Filamu ijayo ya Staa Tom Cruise kuwa imechezwa nje ya Dunia.

Imeelezwa kuwa, Staa huyo ambaye ana uwezo mkubwa wa kufanya "Stunt” zake mwenyewe kwenye filamu, kwa sasa anashirikiana na Billionea Elon Musk pamoja na NASA kwenda kushoot filamu mpya nje ya sayari tunayoishi, Sayari ya dunia.

Kwa mujibu wa Deadline, umeripoti kuwa Staa huyo kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na NASA kuhusu kwenda kutengeneza filamu nje ya anga ya dunia.

Katika hatua nyingine, Billionea wa Kampuni ya "Space X" Elon Musk pia anatajwa kushiriki kwenye mpango huo ambao utaifanya filamu hiyo kuwa ya kwanza kabisa kutengenezwa nje ya dunia.

Sambamba na hilo, hadi sasa bado hazijatolewa taarifa zaidi kuhusiana na filamu hiyo.


EmoticonEmoticon