Netflix Kufuta Account Za Wateja Wote Ambao Hawajazitumia Kwa Muda Huu

Mtandao wa Netflix umetangaza mpango wake wa kuanza kusitisha akaunti za watumiaji ambao wamekuwa kimya 'inactive' kwenye mtandao huo kwa takribani miaka miwili au mwaka mmoja na nusu.

Mpango huo wa urahisishaji unakuja kukusaidia kukumbusha kama unahitaji kuendelea kutumia huduma hiyo au kujitoa. Kuna jumla ya watu milioni 183 ambao akaunti zao hazijalipiwa huduma hiyo muda mrefu, sasa kama wewe ni mmoja wapo, Netflix wametangaza kuanzia wiki hii wataanza kuwatumia email wateja wao, kuuliza kama unahitaji kuendelea katika kifurushi chao au unahitaji kujitoa na kama ukikaa muda mrefu bila kujibu ujumbe huo basi watakuondoa wenyewe moja kwa moja na kusitisha akaunti yako.

Kitu kizuri ni kwamba, endapo utahitaji kurejea tena, taarifa zako utazikuta kama kawaida na vile vitu unavyopenda kutazama.


EmoticonEmoticon