Raisi Wa Marekani Donald Trump Azungumza, Virusi Vya Corona Ndani Ya White House

Wafanyakazi wa Ikulu ya White House wameagizwa kuvaa barakoa wakati wanapoingia jengo la ofisi zake zinazofahamika kama -West Wing, baada ya wasaidizi wawili kupatwa na virusi vya corona.
Wafanyakazi wa White House wamesema kuwa wahudumu wote lazima wavae barakoa wakati wote isipokua wanapokua wameketi kwenye madawati yao ya kazi wakijitenga na wenzao.
Maagizo hayo yanakuja baada ya msaidizi wa Makamu wa rais Mike Pence na msaidisi wa Bwana Trump kuugua.
Bwana Trump anasema anahitaji sera.
Alionekana bila kuvaa barakoa katika bustani ya White House maarufu kama Rose Garden kwa ajili ya mkutano na waandishi kuhusu virusi vya corona , hata hivyo, rais alidai kuwa hahitaji kufuata maagizo hayo kwasababu hukaa "mbali sana na kila mtu", na akapuuza suala la maambukizi ya corona katika White House.
"Tuna mamia ya watu kila siku wanafika White House" kila siku, alisema. "Ninafikiri tunafanya kazi nzuri kuvidhibiti virusi."
Wajumbe watatu watatu wa White House wa kikosi kazi cha kupambana na virusi vya corona walikwenda kujitenga binafsi kwa wiki mbili baada ya kuwepo kwa uwezekano kupata maambukizi ya virusi vya corona.
Ni pamoja na Dkt Anthony Fauci, ambaye amekua maarufu katika vita dhidi ya virusi nchini Marekani.
Afisa habari wa Pence Katie Miller, mke wa mshirika wa Trump Stephen Miller, alipatwa na virusi Ijumaa.
Hii inafuatia kupatikana na ugonjwa kwa mtu anayemvalisha Trump ambaye pia alipatwa na ugonjwa.
Bwana Trump alionyesha kutojali huku akiinua mabega kuhusu kusambaa kwa virusi vya corona katika White House, akisema alikua "kimsingi mtu mmoja " ambaye alipata virusi na mtu huyo amepatikana hana virusi baada ya kupimwa.


EmoticonEmoticon