Rihanna AAngukia Kwenye Orodha Ya Top 5 Wasanii Matajiri Nchini Uingereza

Rihanna ameivamia orodha ya wasanii matajiri nchini Uingereza ambayo inatolewa na Jarida la Sunday Times (Sunday Times Richest List)

Rihanna mwenye umri wa miaka 32 ambaye kwa sasa anaishi nchini Uingereza, ametajwa kuwa na utajiri wa (£468m) sawa na Trilioni 1.3 za Kitanzania.

Utajiri huu umetajwa kutokana na kampuni yake ya biashara ya vipodozi (Fenty Beauty Cosmetics Brand) ambapo inaelezwa kwamba hisa zake ni asilimia 15 na zina thamani ya (£351m) sawa na Bilioni 991 za Kitanzania na kuikamata nafasi ya Tatu.

Hii ni mara ya kwanza kwa Riri kuingia kwenye orodha hii ambayo huwajumuisha wanamuziki wa nchini Uingereza na Utajiri wao kila mwaka. Amewabwaga magwiji kama Sir. Elton John na Mick Jagger.

Nafasi ya kwanza na ya pili zimeshikiliwa na Andrew Lloyd Webber mwenye umri wa miaka 72 na Sir Paul McCartney (77) ambao kwa pamoja wamefungana kwa kutajwa kuwa na utajiri wa TSH. Trilioni 2.2

Top 5 inafungwa na Sir Elton John mwenye utajiri wa takribani TSH. Trilioni 1, na Sir Mick Jagger mwenye utajiri wa TSH. Bilioni 804.7. Mkali Ed Sheeran yupo nafasi ya 10 akiwa na mkwanja unaosoma TSH. Bilioni 565

Mwezi Julai mwaka 2019, Jarida la Forbes lilimtaja Rihanna kama msanii wa Kike tajiri zaidi duniani, akiwa na utajiri wa ($600m) sawa na Trilioni 1.3 za Kitanzania.


EmoticonEmoticon