Shirika La Afya Duniani WHO Limetoa Onyo Kwa Nchi Zinazolegeza Masharti Ya Lockdown

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa angalizo kwa Nchi zinazotangaza nia ya kuondoa ‘lockdown’ ikiwemo Marekani, kwamba zinapaswa kutathmini hali ya corona ilivyo katika Nchi zao kabla ya kuchukua uamuzi huo ili kuepusha madhara zaidi.

"WHO tunashauri mambo sita ya kuzingatia kabla ya kukurupuka kuondoa lock down ikiwemo kuhakikisha maambukizi yamepungua, kudhibiti kasi ya Watu kuambukizana, kufuatilia waliokuwa karibu na wagonjwa, kuzuia maambukizi kuingia nchini kwenu kutoka nje, Jamii ipewe elimu ya kutosha kuhusu corona, kupunguza idadi ya vifo nk, kama hivyo havijafanyika, kuondoa lockdown ni kujitafutia matatizo”- Dr.Tedros, Mkurugenzi Mkuu WHO


EmoticonEmoticon