Shirika La Afya Duniano (WHO) Limeonya Kuwa Huenda Virusi Vya Corona Visiishe

Virusi vya corona huenda ''visiishe''limeonya Shirika la Afya Duniani(WHO)
Akizungumza katika kikao Jumatano, Mkurugenzi wa dharura wa WHO, Dkt Mike Ryan ameonya dhidi ya kujaribu kubashiri ni lini virusi vya corona vitatoweka.
Aliongeza kuwa kama chanjo itapatikana, kudhibiti virusi kutahitaji''juhudi kubwa'',
Takribani watu 300,000 kote duniani wameripotiwa kufa kutokana na virusi vya corona, na zaidi ya visa milioni 4.3 vimerekodiwa.
"Ni muhimu kufahamu hili: Virusi vinaweza kuwa janga jingine katika jamii zetu, na , na virusi hivi huenda visiishe ," Dkt Ryan aliwaambia waandishi wa habari kwa njia ya video kutoka Geneva.
"Virusi vya HIV havijaisha - lakini tumevizowea."
Dkt Ryan amesema pia kwamba haamini "mtu yeyote anaweza kubashiri ni lini ugonjwa huu utatoweka ".
Kwa sasa kuna chanjo zaidi ya 100 zainazofanyiwa utafiti- lakini Dkt Ryan amesema kuna magonjwa mengine, kama vile tetekuwanga, ambayo bado hayajatokomezwa licha ya kuwa kuna chanjo yake.
Mkurugenzi Mku wa Tedros Adhanom Ghebreyesus alisisistiza kuwa bado inawezekana kudhibiti virusi vya corona, kwa juhudi.
"Suluhu liko mikononi mwetu, na ni shughuli ya kila mtu, na sote tunapaswa kuchangia kuzuia janga hili ," alisema.


EmoticonEmoticon