Tahadhari Yatangazwa Juu Ya Uwezekano Wa milipuko Zaidi Ya Corona Marekani

Daktari wa ngazi ya juu wa Magonjwa ya maambukizi nchini Marekani amewaonya maseneta kuwa virusi vitasambaa iwapo nchi itafungua shughuli zake mapema sana.
Dkt Anthony Fauci amesema kuwa miongozo ya shirikisho ya kufungua shughuli za kibiashara tena haitafuatwa , "maambukizi madogo madogo" yatakua mlipuko.
Amesema pia kwamba idadi halisi ya vifo nchini Marekani huenda ikawa kubwa kuliko idadi rasmi inayotolewa ya vifo 80,000.
Ujumbe wake uko kinyume na taarifa iliyotolewa na rais Trump ambaye yuko makini kutaka shughuli za kiuchumi zifunguliwe tena.
Dkt. Fauci alikua akizungumza kwa njia ya video na kamati ya seneti inayoongozwa na Republican nchini Marekani.
Alikua akielezea kuhusu mpango wa kufunguliwa upya kwa shughuli Marekani baada ya majimbo zaidi ya kumi na mbili kuweka amri ya kukaa nyumbani ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona ,ambao unajumuisha awamu ya siku 14 ambazo majimbo yanaombwa kuzifuata wakati wanaporuhusu kufunguliwa kwa shule na biashara.
Majimbo kadhaa ya Marekani ambayo tayari yamekwishaanza tena shughuli zao za kiuchumi yana viwango vya juu vya ongezeko la maambukizi, badala ya kushuka.
Omeonya kuhusu kusababisha mlipuko ambao maafisa hawataweza kuudhibiti, akiongeza kuwa mlipuko wa aina hiyo utarudisha nyuma kufufuka kwa uchumi na unaweza kusababisha "kuugua na vifo".
Ingawa ikulu ya White House imeweka miongozo ya kufungua shughuli za kiuchumi , ni jukumu la magavana kuamua juu ya namna ya kulegeza sharia za kukaa nyumbani zilizowekwa.
"Bila shaka, hata katika hali nzuri sana, ukipunguza hatua za kudhibiti maambukizi utaona visa vinajitokeza ," Dokta Fauchi aliwaonya maafisa wa Mrekani


EmoticonEmoticon