Tekashi69 Amelazimaka Kuihama Nyumba Yake Kisa Jirani Ambaye Ni Shabiki Yake

Tekashi69 amelazimika kuihama nyumba yake baada ya jirani yake kuanika wazi anuani ya nyumba hiyo mtandaoni.

Jirani huyo ambaye ni shabiki wa rapper huyo, alifanikiwa kupenyeza jicho na kurekodi kipande kifupi cha video kikimuonesha 69 aki-shoot video kwenye balcony ya nyumba yake. 

Baada ya hapo alikipeleka mtandaoni na kuambatanisha na anuani ya nyumba, kitendo kilichopelekea watu kuanza kujazana nje na kuleta taharuki na kufifisha usalama wake.

Maofisa wa usalama waliwasili na kuweka ulinzi nje ya nyumba hiyo iliyopo mjini New York, na baadaye ilimlazimu staa huyo wa 'GOOBA' kuwasha ndinga yake aina ya Range Rover ya rangi ya machungwa na kuyahama makazi yake.


EmoticonEmoticon