Trump Akiri Na Kusema Shambulio Kubwa Kuwahi Kutokea Marekani

Trump amesema virusi hivyo vimeipiga Marekani kwa nguvu zaidi ya mashambulio ya mambomu ya Japani katika Bandari ya Pearl katika Vita vya Pili vya Dunia ama shambulio la kigaidi la 9/11 miongo miwili iliyopita.
Utawala wa Marekani kwa sasa unaangazia hatua za adhabu ambazo inaweza kuichukulia Uchina kwa nmana ambavyo walilishughulikia janga hilo katika siku za awali.
Uchina hata hivyo inasema kuwa Marekani inataka kuitumia kama njia ya kuficha mapungufu yao ya nmana gani wamelishughulikua janga hilo.
Toka janga hilo lilipuke katika Mji wa Wuhan mwezi Disemba, virusi vya corona tayari vimeshathibitishwa kuwapata zaidi ya watu milioni 1.2 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 73,000 nchini Marekani pekee.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu yake Tump amesema: "Tumepatwa na shambulio kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini kwetu.
"Shambulio hili ni baya zaidi ya la Bandari ya Pearl. Hili baya zaidi ya la Kituo cha Biashara cha Dunia (9/11). Hatujawahi kupatwa na shambuli kama hili.
"Na halikutakiwa kutokea. Lingeweza kuzuilika kwenye chanzo chake. Lingeweza kuzuiliwa na Uchina. Lingeweza kuzuiliwa kwenye chanzo chake, lakini hilo halikufanyika."
Alipoulizwa iwapo analiona janga hilo kama shambulio la kivita kutoka Uchina, Trump alijibu kuwa kwa sasa adui wa Marekani ni mlipuko wa virusi na si Uchina.
"Ninamchukulia huyu adui asiyeonekana [virusi vya corona] kama vita," amesema. "Sipendi kabisa jinsi gani alifika hapa, kwa kuwa kulikuwa na uwezekano wa kuzuia."


EmoticonEmoticon