Uingereza Yaanza Kutumia Dawa Ya Malaria Kujikinga Na Corona

Jaribio la matumizi ya dawa za malaria kuona kama zinaweza kuzuia ugonjwa wa Corona limeanza nchini Uingereza katika mji wa Brighton na Oxford.
Chloroquine, hydroxychloroquine au placebo zitatolewa kwa wafanyakazi wa afya zaidi ya 40,000 kutoka Ulaya, Afrika, Asia na Amerika ya kusini.
Washiriki wote ni watumishi wa afya ambao wanahudumia wagonjwa wa Covid-19.
Rais Donald Trump alikosolewa baada ya kusema kuwa ametumia dawa ya malaria iitwayo hydroxychloroquine, licha ya angalizo kuwa inawezekana si salama kutumia dawa hiyo kwa ajili ya corona.
Mshiriki wa kwanza, Uingereza katika jaribio la kwanza la kimataifa imesema siku ya Alhamisi katika hospitali ya Brighton na hospitali ya chuo kikuu cha Sussex pamoja na hospitali ya John Radcliffe mjini Oxford.
Watapewa dawa ya hydroxychloroquine au placebo kwa kipindi cha miezi mitatu.
Wakati Asia, washiriki watapewa chloroquine au placebo.
Mipango ya awali ni katika majimbo 25 ya Uingereza na matokeo yanatarajiwa mwishoni mwa mwaka.
Jaribio hilo liko wazi kwa yeyote ambaye anatoa huduma moja kwa moja kwa wagonjwa wenye virusi vya corona nchini Uingereza, ikiwa kama bado hawajapata maambukizi ya virusi vya corona.
Jaribio hili litaangalia kama dawa hizo zitaweza kuzuia wafanyakazi wa afya kupata maambukizi ya virusi vya corona kutoka kwa wagonjwa.
Credit:Bbc


EmoticonEmoticon