Unaweza Kuapata Taarifa Sahihi Na Elimu Kuhusiana Na Corona Kwa Lugha Unayoitaka Kupitia Facebook Ni Rahisi

Kampuni ya Facebook ambayo inamiliki mitandao ya kijamii mbalimbali, hivi karibuni ilizindua sehemu mpya ya kuwaruhusu watumiaji wake kufuatilia taarifa kuhusu virusi vya corona kwenye mtandao wa Facebook.

Toka ilipo anzishwa takribani mwezi mmoja uliopita sehemu hiyo ilikuwa inapatikana kwenye nchi nyingi za jirani na ilikuwa bado haijawezeshwa kwa hapa nchini Tanzania.

Lakini kuanzia siku ya leo sehemu hiyo inasemekana kuanza kuonekana rasmi kwa watumiaji wa Tanzania.
Sehemu hiyo pia inakuja na taarifa za jinsi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona (Common Prevention Tips) ikiwa pamoja na njia salama za kujikinga kwa kufuata kanunuzi za wataalamu wa afya ikiwa pamoja na taarifa nyingine za muhimu.


EmoticonEmoticon