Vipimo Vya DNA Vimevuja, Taarifa Za Future Kukataa Kuwa Yeye Sio Baba Wa Mtoto Zipo Hapa

Ulikuwa ni mvutano wa takribani mwaka mmoja kubaini kwamba Future ni baba halali wa mtoto wa mwanamama Eliza Reign ambaye amekuwa akitoka kwenye mitandao kudai kuwa Future hatoi pesa ya matunzo.

Sasa mambo hadharani, na Future rasmi ni Baba wa watoto 7, mara baada ya kuhalalishwa Reign Wilburn mwenye umri wa mwaka mmoja ni mtoto wake. Hii imekuja baada ya vipimo vya DNA (vinasaba) kuvuja na kuonesha kuwa asilimia 99.99999 Future ndio baba halali.

Juzi (Mei 11) haikuwa siku nzuri kwa Future ambaye aliwatakia heri ya siku ya Mama duniani wanawake wote ambao amezaa nao, kwani alichukizwa na taaarifa za kuvuja kwa vipimo hivyo, alienda twitter na kutapika nyongo kwa hizi tweets tatu.
Eliza Reign alimburuza Future mahakamani akidai pesa za matunzo ya mtoto, aliiambia mahakama kwamba anahitaji kiasi cha TSH. 122.6 Milioni kwa mwezi.


EmoticonEmoticon