Wagonjwa wa Corona Kenya Wafika 1348

Idadi ya maambukizi ya corona iliyothibitishwa nchini Kenya imeongezeka na kufikia 1348. Hii ni baada ya wagonjwa wapya 62 kuongezeka katik muda wa saa 24 zilizopita.

Wizara ya afya imesema kuwa wagonjwa 59 ni vya raia wakenya na raia watatu wa kigeni ambao uraia wao haukuwekwa wazi. Wagonjwa 23 wakiwa wa Nairobi, Mombasa 16, Kwale 8, Kiambu 6, Kajiado 6 na Kitui visa 3. Idadi ya waliopona imefikia 405 baada ya watu 3 zaidi kupona. Vifo ni watu 52.


EmoticonEmoticon