Zambia Yachukua Hatua Ya Kufunga Mpaka Wake Na Tanzania

Zambia imechukua hatua za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona kwa kufunga mpaka wake na nchi jirani ya Tanzania kuanzia Leo Jumatatu. 
Hii ni baada ya kuwa na maambukizi mengi, hususan miongoni mwa wafanyabiashara wa ngono na madereva wa Malori kwemnye miji ya mipaka nchini humo.
Hatua hiyo inajiri baada ya taifa hilo kuripoti wagonjwa 76 wa virusi vya corona katika mji uliopo katika mpake wake na Tanzania
Kufikia sasa taifa hilo limethibitisha wagonjwa 367 wa virusi vya corona nchini humo.
Akizungumza kwa niaba ya rais wa taifa hilo, Edgar Lungu Waziri wa afya nchini humo Chitalu Chilufya alitangaza kwamba mpaka huo utafungwa kwa muda .
Alisema kwamba hatua hiyo itatoa fursa kwa mikakati mipya ya kukabiliana na virusi hivyo kuwekwa.
Katika muda huo, amesema wafanyakazi wa uhamiaji katika mpaka huo watapatiwa mafunzo mapya ya jinsi ya kuhudumia mizigo na raia wanaoingia.
''Hali kule Nakonde ni mbaya na hii leo rais Edgar Lungu ana wasiwasi , Hivyobasi ameagiza kuanzia Jumatatu tarehe 11 mwezi Mei 2020, mpaka wa Nakonde utafungwa kwa muda , hakutakuwa na usafiri ndani na nje ya mpaka huo na vilevile hakutakuwa na usafiri viungani mwa eneo hilo ili kuwezesha utekelezwaji wa mikakati inayolengwa ikiwemo kuwapa mafunzo mafisa wetu mpakani'', alisema waziri huyo wa Afya.
Amesema kwamba maafisa hao vilevile watapatiwa vifaa vya kujilinda dhidi ya ugonjwa huo huku vifaa vya karantini vikiwekwa kwa lengo la kuwalinda maafisa na wakaazi wa Nakonde.
Credit:Bbc


EmoticonEmoticon