August Alsina Arejea Na Album Mpya Baada Ya Kimya Kwa Miaka 5

August Alsina
August Alsina amepanga kurejea na album mpya baada ya kimya cha miaka 5, album hiyo imepewa jina la "The Product III: State of Emergency" na ina jumla ya ngoma 27, imepangwa kuachiwa rasmi June 26 mwaka huu ikiwa na kolabo za Yo Gotti na Tink, pia Lil Wayne na Juicy J.

August Alsina maisha yake ya muziki yaliingiwa na giza mara baada ya kuugua sana ugonjwa ambao aliuita wa kurithi unaopelekea kuathiri kinga yake ya mwili hadi kuharibu mwenendo wa Ini lake, pia alipitia kuumwa jicho lake la kushoto.
August Alsina New Album Cover
Hivyo album hiyo ya tatu itaangazia safari ya maisha yake tangu mtoto mdogo aliyejiingiza kwenye biashara ya dawa za kulevya, kumpoteza baba yake na dada yake, na kuwa muangalizi wa wapwa wake watatu pia mapambano yake na maradhi ya kinga ya mwili ambayo kidogo yachukue uhai wake.
Album Tracklist August Alsina
Kuelekea kuachia album hiyo mpya, Alsina atakuwa akitoa wimbo mmoja kila siku kuanzia June 21 akianza na "NOLA" na kila wimbo utaambatana na episode moja ya documentary yake yenye jumla ya episode 5.

Mwaka 2019 Alsina aliachia wimbo mmoja pekee "TODAY"


EmoticonEmoticon