Bifu Kati Ya Drake Na SwizzBeatz, Kambi Ya Drake Yakataa Msamaha Wa Producer Huyo

Swizz Beatz, Busta & Drake
Ilikuwa usiku mrefu kwa rapper na mtayarishaji Swizz Beatz ambaye alikuwa akizungumza na Busta Ryhmes. Katika mazungumzo hayo Swizz alijikuta akimuita Drake (P*ssy)

Hii ilikuja wakati wakiujadili wimbo wa Busta na Drake ambao ulivuja mtandaoni wiki iliyopita, Swizz bila kificho alizipeleka lawama za kwa Drake akimtaja kuvujisha wimbo huo.

"Kwa sababu mwisho wa siku, jamaa ni K*ma kiukweli. Kwani nini? Tuendelee." Alisema Swizz.

Busta alianza kumuelezea Swizz kuhusu Kolabo hiyo kwamba Drake hawezi kuwa na nia ya kufanya hivyo. Swizz alirudi tena na mashambulizi kwa Drizzy, alimwambia Busta kwamba

"Nguvu zangu zote zimeegemea kwenye hicho kitu ambacho kimevuja mtandaoni na wewe hukuuachia, licha ya mazingira yoyote. Lakini poa. Huyo ni mtoto mdogo tu, sio kwa nia mbaya lakini kama alikuwa amedhamiria basi tungeidungua ndege yake angani." alieleza Swizz.
Kambi ya Drake

Baada ya kauli hiyo, Swizz alijiwahi mtandaoni kuomba radhi lakini kambi ya Drake iliibuka na kumwambia "Hatuhitaji msamaha, ni wazi kwamba hautupendi. Hivyo kuwa hivyo hivyo hata ukituona."


EmoticonEmoticon