Conor McGregor Atangaza Kustaafu Mapambano Ya Ndondi

Mkali wa MMA, Conor McGregor amewashtua mashabiki zake baada ya kutangaza kustaa katika mchezo huo wa mapambano akiwa na umri wa miaka 31.
Mpambanaji huyo wa UFC, kutoka Ireland ametangaza nia hiyo ya kustaafu kupitia akaunti yake ya kijamii ya Twitter hii leo siku ya Jumapili na kuzua gumzo katika mitandao mbalimbali ”Nimeamua kustaafu kupigana.” aliandika McGregor huku akionyesha picha yake akiwa na mama yake huko Las Vegas.
Taarifa hizo za McGregor zimezua gumzo mitandaoni huku wengi wakichukulia kama mzaha tu kutokana na tabia ya nyota huyo kutangaza kustaafu mara kwa mara na kisha kurejea tena kunako ulingo.
Hii sio mara ya kwanza kwa nyota huyo kutangaza kustaafu mchezo wa ngumi, mara kadhaa amekuwa akifanya hivyo, inakumbukwa kuwa hata mwaka jana mwezi Machi aliwahi kusema hivyo na baadaye alirejea tena ulingoni.


EmoticonEmoticon