CORONA : Hatimaye Dawa Kwa Wagonjwa Mahututi Yapatikana

Dexamethasone Covid 19

Dawa ya bei rahisi inayopatikana kwa urahisi Dexamethasone inaweza kusaidia maisha ya wagonjwa wa virusi vya corona waliopo katika hali mahututi.

Wataalam wa Uingereza wanasema kwamba tiba hiyo yenye steroid ni hatua kubwa iliopigwa katika kukabiliana na virusi hivyo hatari.

Inapunguza hatari ya mtu kufariki kwa thuluthi moja miongoni mwa wagonjwa walio katika mashine za kuwasaidia kupumua.

Kwa wale wanaotumia oksijeni inapunguza hatari ya kifo kwa kiwango kikubwa.

Dawa hiyo ni miongoni mwa majaribio ya tiba ya corona duniani kuona iwapo inaweza kusaidia kutibu corona.

Watafiti wanakadiria kwamba iwapo dawa hiyo ingekuwepo nchini Uingereza kuanzia mwanzo wa mlipuko wa corona , hadi maisha ya watu 5000 yangekuwa yameokolewa.

Kwasababu ni ya bei rahisi inaweza kuyasaidia pakubwa mataifa masikini yanayotatizika katika kukabliana na ugonjwa wa Covid-19.


EmoticonEmoticon