CORONA : Mamilioni Ya Wakazi Wa Beijing Waamriwa Kutotoka Nje Ya Jiji

mjini Beijing
Mamilioni ya watu mjini Beijing wanaishi chini ya masharti mapya, wakati idadi ya watu walioambukizwa virusi ikiendelea kuongezeka.
Mji huo uliripoti kuwepo kwa wagonjwa 31 siku ya Jumatano na kufanya idadi ya wagonjwa kwa kipindi cha juma lililopita kufikia 137.
Kabla ya ongezeko kubwa, mji huo mkuu wa China kwa siku 57 haukuripotiwa kuwa na mgonjwa hata mmoja.
Mlipuko huo unaaminika kuanzia kwenye soko la chakula la Xinfandi ambalo husambaza 80% ya vyakula vya nyama na mboga mboga katika mji huo.


EmoticonEmoticon