CORONA : Watu 97 Wameruhusiwa Kwenda Nyumbani Baada Ya Kupata Nafuu Dhidi Ya Corona

Kenya Covid 19
Katika msimamizi katika wizara afya Dr Rashid Aman amesema serikali ya Knya imewaruhusu watu 97 zaidi kuondoka hospitalini baada ya kupata nafuu kutokana na virusi hivyo hatari.

Takwimu hizo mpya sasa zinafanya watu waliopona nchini kutokana na virusi vya corona kufikia 849.

Aman pia amesema taifa litaendelea kurekodi idadi kubwa ya watu walioathirika na virusi hivyo kutokana na hatua ya serikli ya kuendelea kuwapima watu wengi.

Amewataka wakenya kuendelea kuvalia barakoa na kuosha mikono kila siku ili kupunguza maambukizi.

Ameongezea kuwa chini ya saa 24,watu 95 wamepatikana na virusi vya corona.

Wakenya ni 92 huku watu watatu wakiwa raia wa kigeni.
‘Mombasa imesajili watu 56 kati ya visa hivyo vipya huku Nairobi ikiwa na visa 13.

Kati ya 10 vilivyosajiliwa kaunti ya Busia,watu 9 ni madereva wa Malori ya kubeba mizigo.

Kufikia sas kenya ina wagonjwa 2862 wa virusi hivyo.
Aidha mgonjwa mmoja mmoja amefariki na kufikisha watu 85 waliofariki.

Maafisa wa afya watatu katika kaunti ya Nyeri wamedhibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.

Kati ya visa hivyo vipya vilivyosajiliwaa hii leo,wanaume ni 56 huku wanawake wakiwa 38.

Jimbo la Marsabit limekuwa la hivi karibuni kusajili kisa kwanza kuhusiana na corona na kufikisha idadi ya kaunti 38 zilizoandikisha maambukizi.
Credit:Radiojambo


EmoticonEmoticon