CORONA : WHO Yatahadharisha Kuwa Hali Ya Maambukizi Itakua Mbaya Zaidi Siku Za Usoni

Tedros Adhanom Ghebreyesus
Hali bado inaweza kuwa mbaya zaidi wakati huu wa janga la Covid-19, Shirika la afya duniani (WHO) limetahadharisha, miezi sita ikiwa imepita tangu mlipuko wa ugonjwa huo kutokea.

Mkuu wa shirika hilo, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema virusi vinaweza kuathiri watu wengi zaidi ikiwa serikali hazikuanza kutekeleza sera sahihi.
Ujumbe wake ulibaki kuwa ''Pima, fuatilia, tenga na weka karantini'', alisema.
Zaidi ya watu milioni 10 wamethibitishwa kuwa na maambukizi duniani tangu virusi hivyo vilipojitokeza nchini China mwishoni mwa mwaka jana.
Idadi ya wagonjwa waliopoteza maisha sasa ni zaidi ya 500,000
Nusu ya idadi ya watu walioambukizwa duniani imekuwa Marekani na Ulaya, lakini idadi inaongezeka kwa kasi Amerika.
Virusi hivyo pia vinaathiri Kusini mwa Asia na Afrika, ambako hakutarajiwi ongezeko la juu mpaka mwishoni mwa mwezi Julai.
Dkt Tedros akitoa hotuba yake siku ya Jumatatu alisema: ''Sote tunataka hali hii kuisha. Sote tunataka kuendelea na maisha yetu. Lakini ukweli ulio mchungu ni kuwa bado hali hii haijafikia kuisha hata kidogo''
'' ingawa nchi nyingi zimepiga hatua, bado ugonjwa huu unashika kasi duniani.''
''Kukiwa na wagonjwa milioni 10 sasa na vifo vya watu nusu milioni, mpaka pale matatizo yaliyogundulika yatakajulikana na WHO, ukosefu wa umoja wa kitaifa na kidunia na dunia iliyogawanyika hali inayosaidia kusambaa kwa virusi…bado hali itakuja kuwa mbaya zaidi,'' alisema.
''Samahani kwa kusema hivyo, lakini kwa mazingira ya namna na hali hii, tunahofu hali kuwa mbaya .''
Amezitaka serikali kufuata mifano ya Ujerumani, Korea Kusini na Japan, ambazo zimekuwa zikichukua hatua kudhibiti maambukizi kwa kutumia sera ikiwemo vipimo na ufuatiliaji.


EmoticonEmoticon